NA ZAINAB ATUPAE

KOCHA wa klabu ya Malindi SC Mohamed Badru Juma  amesema wanatarajia kuanza rasmi mazoezi kwa siri kujiandaa na ligi kuu ya Zanzibar .

Akizungumza na gazeti hili kocha huyo alisema mazoezi hayo yatasaidia kuficha mbinu ambazo atazitumia kuwapa wachezaji wake.

Alisema awali alikuwa akifanya mazoezi ya mchujo wa kutafuta wachezaji wa kuwasajili ili kuogeza  nguvu katika kikosi chake.

Alisema katika kujiandaa na ligi hiyo mategemeo yao kucheza mechi nne hadi tano za kirafiki na timu zinazoshiriki  ligi kuu ya Zanzibar.

“Kwenye mchujo tulicheza mechi nyingi za kirafiki na timu za madaraja ya chini, lakini hivi sasa tutacheza na mechi za madaraja ya juu,”alisema

Alisema lengo ni kuijenga  timu hiyo kurudi kama ilivyo kuwa awali,hivyo aliwataka wachezaji,viongozi kushirikiana ili kufikia malengo yao msimu huo.

Aidha aliwataka wachezaji kuwa pamoja na viongozi na kufuata maelekezo yote wanayopewa katika kuhakikisha wanaleta mabadiliko kwenye timu yao kuelekea msimu mpya.