NA MWANDISHI WETU

HUENDA kuna mijadala mingi kuhusu ni nani aliyewahi kuwa mchezaji bora zaidi katika soka duniani.Je ni Maradona,Messi Ronaldo au Cruyff.

Akiwa mzaliwa wa Tres Corazones, mji uliopo takriban kilomita 200 mashariki mwa mji wa Sao Paulo, Brazil tarehe 23 mwezi Oktoba 1940, Pele alivunja rekodi zote, hata iwapo alionesha mchezo mzuri wakati ambapo soka ilikuwa ikipimwa kulingana na kipaji chake na sio magoli aliyofunga.

Alifunga zaidi ya magoli 1200 na kuwa mfungaji bora wa timu ya Brazil, pia alifunga idadi kubwa ya (Hatrick): 92.

Alikuwa mchezaji mwenye namba dogo zaidi kushinda kombe la dunia. Na ndie mchezaji wa pekee kushinda makombe matatu tofauti ya dunia. Sweden 58, Chile 62 and Mexico 70.

Hio ndio sababu alipokea zawadi chungu nzima kama vile mchezaji bora wa karne ya 20 na mchezaji bora wa soka katika karne ya 20.

Hata hivyo uchezaji wake wa miongo mitatu ni miongoni mwa vyanzo vya masuala mengine ambayo huyajui kumhusu Pele ambaye sasa anatizima miaka 80 wiki hii.

  1. Alikuwa mlinda mlango mara nne na aliisaidia timu yake kufika fainali.

Alikuwa mchezaji aliyetumia mguu wa kulia lakini mengi ya mabao yake 400 aliyafunga kwa kutumia mguu wa kushoto.

Pia alicheza kama mlinda lango mara nne: Mwaka 1959, 1969 and 1973.lakini mwaka unaokumbukwa sana ni 1963.

Santos ilikuwa anapinga mechi ya nusu fainali ya kombe la Brazil dhidi ya klabu ya Porto Alegre Gremio. Mechi hiyo iliisha 4-3, kufuatia (hatrick) iliofungwa na Pele.

Hata hivyo kunako dakika ya 86, Gilmar, mlinda lango wa Santos alipigwa kadi nyekundu na kutoka nje na hakuna wachezaji wa ziada walioruhusiwa uwanjani.

Nani aliyekwenda kulinda lango hilo? alikuwa ni Edson Arantes Pele.

Mwisho wa mechi Santos ilifaulu kutinga fainali ya kombe la Brazil ambapo hatimaye timu hiyo iliibuka mshindi.

2. Ni mchezaji wa pekee aliyesababisha refa kupewa kadi nyekundu na kuruhusiwa kucheza tena baada ya kutolewa nje.

Tukuio hili lilifanyika nchini Colombia. Santos ilikuwa timu bora katika Amerika , lakini pia ilikuwa ikizuru mataifa tofauti duniani kumuonesha nyota wake.

Tarehe 17 mwezi Julai 1968 mjini Bogota. Usiku huo, Santos ilicheza dhidi ya timu ya michezo ya Olimpiki ya Colombia.

Mechi hiyo haikuwa ya kuvutia . Refa, Guillermo Velasquez alipigana na mchezaji mmoja na dakika chache baadaye Pele aliomba kupatiwa mkwaju wa Penalti.

Velásquez alidai kwamba katika mahojiano toafuti Pele alimuonesha ujeuri .Na alielewa ;lakini akaamua kumpatia kadi nyekundu.

Pele alikubali akatoka.Kulingana na vyombo vya habari , Wachezaji wa Santos walimshambulia refa Velasquez kwa ngumi , wakamtoa na kumbadilisha na mshika bendera mmoja aliyekuwa msaidizi wa refa huyo ambaye alilazimika kutumia kitambaa cha kujifuta uso kama bendera.

Pele alirudi uwanjani kufuatia maombi ya mashabiki. Mechi hii iliisha 4-2 Santos wakiibuka washindi.

”Kati ya wachezaji 28 walioletwa na Santos 25 walinipiga . Wale ambao hawakunipiga ni Daktari na mwandishi kutoka Folha de São Paulo na Pelé,” Velásquez alisema miaka kadhaa baadaye.

3. Alivunja pua ya mpinzani wake kwa kichwa na ni kitu ambacho alijutia kwa muda mrefu.

Picha nyingi za Pele zinamuonesha kama mtu anayetabasamu na mpenda watu. lakini uwanjani hali ilikuwa tofauti kabisa.

Mojawapo ya matukio ambayo Pele anajuta kufanya yalifanyika wakati wa mechi kati ya Brazil na Argentina katika kombe la kitaifa 1964.

Kinyanganyiro hicho kilichezwa nchini Brazil na ilitarajiwa kwamba ni taifa la Brazil litakaloibuka mshindi.

Walikuwa wamewakaribisha Portual, England na dakika ya mwisho waliitaka Argentina pia wajumuike ili kukamilisha kundi la nchi zitakazoshiriki.

Katika mechi ya pili, Pele akiwa mshambuliaji ilicheza dhidi ya wapinzani wao wakuu Argentina.

Mkufunzi wa Argentina Jose Maria Minella alimweka beki Jose Agusti Mesiano kumkaba pele.

Mesiano mara kwa mara aliweza kumzuia nyota huyo. Alimkaba Pele kila safu hivyobasi kutoweza kupata pasi.

Pele alipoona kwamba amekabwa sana hata hawezi kupumua hatua ambayo ilimzuia kuisaidia timu yake kuepuka kichapo alibadilika kutoka mjumbe wa amani hadi kuwa yule wa vita.

“Alikasirika kwa sababu nilimfuata kila mahali. Mchezo ulikuwa mbaya. Nilimpokonya mpira na kumpatia Varacka na mara moja nikahisi ngumi imenipiga usoni. Nilianguka, nikaona damu inatiririka puani”, alimwambia miaka mingi baadaye, Mesiano aliambia gazeti la Argentina Ole, huku akionesha kovu alilomuachia katika pua yake.

Refa ambaye alikuwa akishughulikia suala jingine tofauti hakuona kilichofanyika hivyo basi hakuwezi kumtoa nje nyota huyo wa Brazil.

Miaka michache baadaye, katika mahojiano Jarida la Argentina El Grafico, Pele alikiri kwamba hilo ndio tukio analojutia sana katika kipindi chake chote cha soka uwanjani. Anasema kwamba baadaye aliomba msamaha.

4.Amekuwa muigizaji katika filamu 10 mojawapo akishirikiana na Sylvester Stallone pamoja na Michael Caine. Kitu kimoja ambacho hakijajulikana kuhusu Pele ni kuwa muigizaji na mwimbaji.

Katika rekodi za Filamu Edson Arantes do Nascimento Pele anaonekana kama muigizaji katika filamu 10 na kipindi kimoja cha runinga.

Filamu iliokuwa maarufu ni ile ya “Escape to Victory” mwaka 1981, ambapo alielekezwa na John Huston na kushirikiana na nyota wawili washindi wa tuzo za Golden Globe winners: Sylvester Stallone na Michael Caine.

Haijulikana iwapo Huston ilivutia kutokana na ushirika wa Pele. Pia aliigiza katika filamu kama vile Solidão, Uma Linda Historia de Amor , ” Pedro Mico” na katika filamu ya kihistoria ya A Marcha , mwaka 1972.

Na hakuigiza pekee kwani pia aliimba akishirikiana na Elis Regina miaka ya 60 na albamu ya 2006 kwa jina Ginga.