LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester United, Marcus Rashford alifunga mabao matatu, (hat trick) akitokea benchi wakati mashetani wekundu wakiichapa RB Leipzig kwa bao 5-0 katika mchezo wa kundi H.

Rashford aliingia dakika ya 64 akichukua nafasi ya Mason Greenwood ambaye alifunga bao na kupachika mabao dakika za 74, 78, na 90.

Mabao hayo matatu yanamfanya Rashford kuwa kinara wa ufungaji akiwa amefikisha mabao manne katika mechi mbili alizocheza.

Mabao mengine ya Manchester United yalifungwa na Mason Greenwood na Antony Martial aliyepachika kwa mkwaju wa penati dakika ya 87.