TOKYO,JAPAN

MANUSURA wa mashambulio ya bomu la atomiki ya mwaka 1945 nchini Japani wanasema wataendelea kukusanya saini za kampeni inayotoa wito kwa nchi zote kujiunga na mkataba wa Umoja wa Mataifa unaopiga marufuku silaha za nyuklia.

Maofisa wa Nihon Hidankyo, yaani Shirikisho la Japani la Mashirika ya Waathiriwa wa Bomu la Atomiki na Haidrojeni, walifanya mkutano na wanahabari jijini Tokyo .

Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba Mkataba wa Kupiga Marufuku Silaha za Nyuklia utaanza kutekelezwa Junuari 22, 2021, ikiwa ni siku 90 baada ya kuidhinishwa na nchi 50 zilizohitajika ili utekelezwe.

Mwenyekiti mwenza wa Nihon Hidankyo Tanaka Terumi alisema anafurahi sana kuwa mkataba huo utakuwa sheria ya kimataifa.

Akigusia kwamba Japani bado haijajiunga na mkataba huo, Tanaka alisema atafanya kila awezalo ili serikali ibadili sera yake kabla ya mkataba huo kuanza kutekelezwa.

Mataifa yenye nguvu ya nyuklia ikiwemo Marekani hayajaidhinisha mkataba huo.