YEREVAN, ARMENIA
VIKOSI vya Armenia na Azerbaijan vimeshambuliana kwa maroketi na makombora wakati ambapo mapigano yanazidi kwenye eneo la Nagorno-Karabach.
Armenia ilisema kuwa mji mkuu wa Nagorno-Karabach, Stepanakert ambao ulikuwa ukishambuliwa kwa makombora ulishambuliwa tena.
Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan ilisema vikosi vya Armenia viliushambulia mji wa Ganja, huku picha zikionyesha kuharibiwa vibaya kwa majengo.
Hikmet Hajiyev, mshauri wa Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba vikosi vya Armenia vilianzisha mashambulizi ya makombora dhidi ya raia wa Azerbaijan na miundombinu ya raia, kwenye mji wa Mingechavir, umbali wa kilomita 80 kutoka kwenye mji mkuu, Baku.
Nchi hizo mbili zilipinga wito wa kimataifa wa kusitisha mapigano na badala yake zilizidisha mapigano katika siku za hivi karibuni, huku kila upande ukitangaza kushinda