WASHINGTON, MAREKANI

MAMLAKA ya Jeshi la Anga nchini Marekani imetangaza kufanya majaribio ya kombora aina ya “Minuteman III” linaloweza kubeba nyuklia na kusafirisha angani.

Kwa mujibu wa maelezo yalitolewa na mamlaka hiyo, iliarifiwa kuwa kombora hilo lililojaribiwa kwenye kambi ya jeshi la anga ya Vandenberg iliyoko California, halikubebeshwa nyuklia wakati wa majaribio.

Maelezo zaidi yalibainisha uwezo na nguvu kubwa ya kijeshi iliyokuwa nayo Marekani na kuthibitisha kuwa ni tishio kwa kipindi hiki cha karne ya 21.

Chombo kilichotumiwa kubeba kombora hilo hewani, kilisafiri kwa masafa ya maili 4,200 angani hadi kufikia kisiwa cha Kwajelin.

Mamlaka ya jeshi pia ilichapisha picha za urushaji wa kombora hilo katika mtandao wa kijamii.