LONDON, England

MASHABIKI wa soka nchini Uingereza wanaweza kurejea tena viwanjani hivi karibuni, baada ya ombi la mashabiki kupata saini nyingi kutoka kwenye Bunge la Uingereza ambalo limepanga kuijadili taarifa hiyo Novemba 9, mwaka huu.

 Tangu Machi, Serikali ilipiga marufuku mashabiki kuingia viwanjani kutokana na ugonjwa wa Corona, hivyo hatua hiyo endapo itafikiwa ni nafuu kwa Klabu nyingi ambazo zinategemea zaidi mapato ya mlangoni kuendesha klabu zao.

Licha ya kuchezwa bila ya mashabiki, ligi hiyo imeendelea licha ya ukweli kuwa  imepungua msisimko na ladha, ambapo mpaka sasa zimechezwa raundi tano.