KAMPALA,UGANDA

MARAIS wa nchi nne wamekubaliana kuongeza juhudi za kuimarisha usalama katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika mbele ya vikundi vyenye silaha na uporaji wa maliasili.

Ofisi ya rais wa Congo ilisema,mazungumzo hayo, yaliahirishwa mara mbili kwa sababu ya kutokubaliana juu ya ajenda na muundo, yalikusanya wakuu wa Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda na Uganda, ambao walizungumza kwa njia ya video.

Walikubaliana kupunguza vyanzo vya ufadhili kutoka vikosi hasi,taarifa ya pamoja ilisema baada ya mkutano huo mfupi, katika kumbukumbu dhahiri kwa wanamgambo mashariki mwa DR.

Marais wanne hao pia waliahidi kupambana kwa pamoja na mitandao ya magenge,kikanda na kimataifa,ambayo inachangia unyonyaji na biashara haramu ya maliasili.

Rais Felix Tshisekedi alishiriki katika mkutano huo kutoka Goma,mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini,ambapo mamia ya watu waliuawa kwa mwaka jana na Kikosi cha Allied Democratic Forces (ADF), wanamgambo ambao walitokea miaka ya 1990 kama waasi Waislamu wa Uganda.