NA HABIBA ZARALI, PEMBA

MGOMBEA Ubunge jimbo la Mkoani, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amewataka wananchi wa jimbo hilo kumpa ridhàa ya kushika nafasi hiyo, ili aweze kuwatatulia changamoto zinazowakabili ikiwemo ya ajira na kuwaletea

maendeleo mbalimbali katika jimbo lao. Alisema tatizo kubwa la wananchi jimboni humo ni maendeleo, hivyoatakapopata ridhaa atahakikisha maendeleo katika jimbo hiloyanapatikana kwa haraka. Profesa Mnyaa, alieleza hayo, katika mkutano wa kampeni uliofanyika

katika viwanja vya Garden Shehia ya Mbuyuni jimbo la Mkoani Kisiwani Pemba. Alifahamisha aliamuwa kugombania nafasi hiyo, ili aweze kuwatatulia

changamoto zinazowakabili kwani waliowachaguwa miaka ya nyuma hakuna maendeleo waliyoyafanya.

” Mimi ndie yule Mbarawa ambae nina uchungu wakuwaletea wananchi wajimbo la mkoani maendeleo naomba munichaguwe”,alisema.

Akizungumzia kura ya mapema alisema si ya watu wote ni ya watu maalum na ipo kisheria, hivyo ni vyema kufuata utaratibu ili zoezi liwezekwenda kwa usalama na amani.

Kwa upande wake mgombea Uwakilishi jimbo la Mkoani, Capt, Abdalla Hussein Kombo, alisema,  atakapopata ridhaa atahakikisha anazitengeneza barabara za ndani zote kwa kiwango cha lami.

Mnyaa, alieleza atahakikisha kuwa anashirikiana na Serikali ya awamu ya nane kuvifanyia utambuzi bandari ya Mkoani, ili iweze kupokea meli za kimataifa.

Akizungumzia fursa kwa  vijana wa Mkoani alisema, akipata ridhaa watasomeshwa ubaharia, ili waweze kuvua kitaalamu tena kwa meli za nje ambazo zitawawezesha kupata faida kubwa kuliko sasa.

Mapema akifunguwa mkutano huo Katibu wa CCM Wilaya ya Mkoani Mohamed Abdalla Ali, alisema Wilaya ya Mkoani, imeimarika kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi hivyo ni vyema wananchi wakachaguwa viongozi haowatakaoweza kuendeleza sera za Chama hicho.