WOLLONGONG, Australia

MWANASOKA mkongwe wa Uingereza atastaafu soka baada ya kucheza mechi yake ya mwisho ya kimashindano siku ya Ijumaa akiwa na umri wa miaka 80.

Peter Webster anaeishi Wollongong nchini Australia amesema ametambua kwa muda sasa, kuwa hatoweza kuwa na mchango kama alikuwa nao zamani .

Alianza kucheza mechi za kimashindano akiwa na umri wa miaka 15, japokuwa alisoma skuli ambayo mchezo wa soka haukuwa umetawala zaidi.

Brewster alicheza timu nyingi za ligi ya Wales alipokuwa na miaka 20 na 30 kabla ya kuhamia Australia na mke wake Moira pamoja watoto wake watatu mwaka 1981.

Nyota huyo amesema ameshangaa kuona soka la Australia limekuwa sana ”ni bora kucheza kwenye sehemu yenye joto la celsius 38 kuliko farhrenheit 38.”

Pia anatamani kuwaangalia wajukuu zake wakicheza soka katika kipindi cha ustaafu wake.mke wake anahitaji kuona mumewake akifanya shughuli mbalimbali nyumbani.

Webster amepanga kuwasili mapema kwa ajili ya mechi ya siku ya Ijumaa usiku dhidi ya Russell Vale vinara wa ligi hivyo anaweza kuongeza goli.

Pia amewataka wapinzani kutambua kuwa haitokuwa rahisi hivyo wasimchukulie rahisi.

Bwana Webster ni gwiji ambaye anafahamika hata katika soka la mtaani na kuna mashindano ya soka yaliyopewa jina lake Peter Webster Cup.

Kuhusu mashindano hayo amesema”kwa kawaida ni lazima ulipie lakini kwa mimi sitotaka kulipwa chochote na kwakuwa bado niko hai natamani siku moja kucheza mashindano hayo”

Webster amesema amekaa muda mrefu bila kucheza na hana uhakika atajisikiaje baada ya mechi yake ya mwisho.