NA ABDI SULEIMAN

MGOMBEA uwakilishi wa jimbo la Ole kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Massoud Ali Mohameda, amewaomba  wananchi wa jimbo hilo kuhakikisha wanamchagua ili awaletee maendeleo.

Alisema hayo katika mkutano wa kampeni wa jimbo hilo uliofanyika juzi.

Aliwaomba wazee na wenyeji wa jimbo hilo kuhakikisha hawapotezi kura zao kwa kuwachagua wapinzani.

 “Nimekuja kwenu kuwaomba kura mnichague niwe mwakilishi wenu, ili niwatumikie,” alisema.

Alisema wakati umefika sasa kwa wananchi wa jimbo hilo kubadilika kwani miaka zaidi ya 20 wamekuwa wakichagua wapinzani.

Kuhusu ujasiriamali, aliwahakikishia kuwapatia mikopo ambayo haitakuwa na riba.