ZASPOTI
IMEAMULIWA kuwa Misri itakuwa wenyeji wa fainali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF ya 2020 iwapo timu ya taifa hilo na nyengine kutoka Morocco zitatinga fainali baada ya ‘droo’ uwanja utakaotumika kufanyika juzi.


Wydad walitarajiwa kukutana na Al Ahly wakati Raja watacheza na Zamalek jijini Casablanca, Morocco katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali.
Mechi za marudiano zitachezwa Oktoba 23 na 24 katika uwanja wa kimataifa wa Cairo jijini Cairo.
Mchezo wa fainali ulikuwa haujaamuliwa kabla ya Ijumaa, wakati ‘droo’ ilipofanyika Casablanca nchini Morocco. Droo hiyo ilikuwa kati ya Misri na Morocco na ilikuwa ndiyo aliyochaguliwa kama mwenyeji wa mechi.


Hata hivyo, CAF, ilisema kwamba ikiwa timu mbili kutoka nchi moja zitafuzu fainali, mchezo utachezwa katika nchi yao.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF inaweza kujiunga na hafla kadhaa kuu katika soka ya Afrika kuandaliwa na Misri kwa muda mfupi, baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 na Kombe la Vijana chini ya umri wa miaka 23 mwaka 2019.(Goal).