NA MARYAM HASSAN

MRADI wa ujenzi wa mji wa kisasa wa kwahani unatarajiwa kuzinduliwa rasmi leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein ikiwa ni utekelezaji wa ilanai ya uchagfuzui ya ccm na mipango ya maendeleo ya zanzubar.

Ujenzi wa mji huo ulioanza mwaka jana na kuwekewa jiwe la msingi mwanzoni mwa mwaka huu wakati wa sherehe za mapinduzi ya zanzibar, unatarajiwa kuwa ni miongoni mwa miji ambayo serikali ya mapinduzi zanzibar imepanga kuijenga.

Miji mingine iliyopo katika mipango ya serikali ni pamoja na mji wa Chumbuni, chwaka na sehemu yote ya ng’ambo ya zamani ambayo ili kuendeleza sera ya makazi bora iliyoasisiwa na rais wa kwanza wa zanzibar marehemu Abeid Amani Karume.

Hivi karbuni, wakati akifungua jengo la maduka ya kibishara la ‘Michenzani Mall’, dk. Shein alieleza kuwa uzinduzi wa nyumba hizo ni miongoni mwa miradi mikubwa iliyosimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya jamii (ZSSF), ambayo ina lengo la kuipa hadhi mji wa Zanzibar.

Hivyo aliwataka wananchi kujitokeza na kushudia mafanikio ya utekelezaji wa mipango ya serikali Mapinduzi ya Zanzibar kwa kusimamia vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi.