NA ZAINAB ATUPAE

KOCHA mkuu wa timu ya Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa amesema Zanzibar ina vijana wenye vipaji, lakini tatizo wamekosa nguvu  na pumzi za kupambana  wakati wanapokutana na timu kubwa kama za Tanzania Bara.

Mkwasa aliyasema hayo hivi karibuni  huko Mao Zedong wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili, baada ya kumaliza mechi ya kirafiki waliocheza na timu ya Jang’ombe boys na Ruvu kuondoka na ushindi wa mabao 3-1.

Alisema  Zanzibar kuna vipaji  na wachezaji wana ari ya kucheza,lakini kinachokosekana ni mazoezi nguvu kama wavyopewa wachezaji wa timu za Bara.

Alisema kwa kuliona hilo aliwashauri viongozi wa timu kuanzia za madaraja ya chini kuwapa mazoezi ya nguvu kama kukumbia kuwapeleka kwenye fukwe ambapo yatawasaidia kupata nguvu katika miguu yao.

“Mchezaji utakapo muandaa tokea mapema basi hata anakokwenda atafanya vizuri na ndio nikawataka waanze huku chini na juu kumaliza,”alisema.