LONDON, England

JOSE Mourinho,  Kocha Mkuu wa Spurs amesema kuwa miongoni mwa timu ngumu kucheza nazo ndani ya Ligi Kuu England ni pamoja na klabu ya Manchester United.

Mourinho aliweka rekodi ya kuitungua mabao 6-1 timu yake ya zamani kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa wikiendi ambao umemuweka matatani mrithi wa mikoba yake Ole Gunner Solskjaer.

Kwa sasa inaelezwa kuwa mabosi wa Manchester United wapo kwenye mchakato wa kumpata mrithi wake huku Mauricio Pochettino aliyekuwa akiinoa Spurs akitajwa kuwa kwenye hesabu za kuibukia kikosi hapo.

Mourinho amesema:”Moja ya timu ngumu kucheza nazo ndani ya England ni pamoja na Manchester United,  ni ngumu kucheza nao na kupata ushindi kwa uhakika ndani ya dakika 90.

“Ugumu wake ni kwamba unaweza ukawashinda ndani ya uwanja baada ya dakika 90 lakini huwezi kupata furaha ya kushangilia huo ushindi mpaka ufike nyumbani kwa kuwa unaweza kushangaa upo ndani ya chumba cha kubadilishia nguo mwamuzi anakufuata na kukwambia mwambie kipa wako ajiandae Bruno Fernandes anakwenda kupiga penalti.”