NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Kikosi cha Yanga SC, Waziri Junior amesema ndio kwanza ameanza kufanya majuku yake kama mshambuliaji , kila atakapo pata nafasi lazima afunge.

Waziri juzi aliifungia klabu yake ya Yanga bao la moja ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo tangu ajiunge hapo.

Walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi yta timu ya KMC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la CCM Kirumba bao la pili likiingizwa kimiani na Tuisila Kisinda.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana, Waziri alisema amefurahi sana kupata nafasi nakufunga hilo alilipanga tangu anatoka kambini kwamba nilazima afunge kwenye mchezo huo.

Alisema anataka kuingia kwenye ushindani wa ufungaji bora na ikiwezekana achukue kiatu cha msimu huu ambacho msimu uliopita kilichukuliwa na Kagere na msimu huu wamejitokeza wengi wenye kuleta ushindani kwenye ufungaji.

“Nimefurahi kufunga na nimefurahia pia kumfunga Juma Kaseja, Ndoto zangu nikuhakikisha nakuwa mfungaji bora waligi panapo majaaliwa,” alisema