ANKARA,UTURUKI

MVUTANO kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki umeongezeka zaidi baada ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuhoji hali ya kiakili ya mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Maofisa kadhaa wa Umoja wa Ulaya walikosoa vikali matamshi ya Erdogan na Halmashauri Kuu ya Ulaya na kusema kuwa kiongozi huyo wa Uturuki anapaswa kubadilisha mtizamo wake ikiwa anataka juhudi za jumuiya hiyo za kuanzisha upya mazungumzo na nchi yake ziendelee bila vikwazo.

Erdogan alisema Macron anahitaji kupimwa akili wakati akijibu kauli za rais huyo wa Ufaransa kuhusu matatizo yanayowekwa na Waislamu wa itikadi kali nchini Ufaransa ambao wanamfuata Macron.

Katika hatua isiyo ya kawaida, Ufaransa ilimuita balozi wake kwa mashauriano.

Uturuki pia ilitoa wito wa kususia bidhaa za Ufaransa, Msemaji wa Umoja wa Ulaya Peter Stano alisema kuna uwezekano wa kuitishwa mkutano wa dharura wa mawaziri wa EU kufuatia kauli za karibuni za Erdogan.