Akampeni za kisayansi zamuwezesha kujua mengi

HAJI NASSOR NA THUREA GHALIB, PEMBA

MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi, amesema chama hicho kina kila sababu ya kupata ushindi kutoka na kufanya kamapeni za kistaarabu na kisayanasi.

Aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa, makada wa chama cha Mapinduzi, mabalozi wa wenyekiti wa mashina, ukumbi wa skuli ya sekondari ya Fidel Castro ilaya ya Chake Chake, Mkoa wa kusini Pemba.

Alisema kwa kushirikiana na wenzake wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha kampeni za chama hicho zinakuwa bora na imara kwa kule kuyafikia makundi yote ya wananchi wa Zanzibar.

Alisema, hilo na mengine ndio ambayo yatakihakikisha chama cha Mapinduzi kinaibuna na ushindi usio na malalamiko, kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Alieleza kuwa, wamekuwa wakikutana na makundi kama ya wafugaji, wavuvi, wajasiriamali, mama lishe, wafanya wa taasisi za umma jambo ambalo limewavutai mno wananchi hao.

“CCM kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi huu, ushindi unakuja na hauna wasi wasi, maana tumekuwa tukifanya kampeni za kisayansi na kiungwana ambazo hazina viashiria vya uvunjifu wa amani,’’alisema.

Katika hatua nyingine mgombea huyo wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Hussein Mwinyi, alisema kila mwanachama wa chama hicho, lazima ahakikishe ifikapo Oktoba 28, anajitokeze kukipigia kura chama chake.

Alisema haya wale wa vyama vyengine iwe ni ACT-Wazalendo, CHADEMA, CUF, AAFP, NRA, ADC, UPDP ni vyema wakawapigia kura wagombe wote wa CCM ili chama cha mapinduzi kuleta mandeleo.

Mgombea huyo alitakata Viongozi wa Chama Kuhakikisha kuwa waWAnandaa Mabalozi kufanya majukumu yao, endapo kutakua na changamoto zozote basi wasisite kuzielezea ili wapate kusaidiwa.

Akizungumzia kuhusu suala la kuleta maendeleo Dk. Hussein alisema kuwa amezamiria kufanya mapinduzi makubwa ya uchumi hapa Zanzibar, ili kuwaletea maendeleo wananchi wote.

Akizungumzia sula la amani Dk. Hussein aliwasihi wananchi kutunza na kuendelea amani waliyonayo, na wasikubali kurubuniwa na baadhi ya watu wasioiakia mema nchi.