NA MWANDISHI  WETU, ZANZIBAR 

MWANASIASA Mkongwe Zanzibar, Mzee Ali Ameir Mohamed, amesema  mgombea Urais wa CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi. ni mwanasiasa makini , na mwenyeuwezo wa kuchapakazi vizuri, kwani ameandaliwa kusimamia mageuzi ya kimaendeleo.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mzee Ali Ameir Mohamed, mara baada ya kumalizika mkutano  wa hadhara wa kamepeni za Urais Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja. 

Alisema mgombea huyo  ameonesha anaelewa vyema miundo ya uendeshaji utawala   kisera  , kifalsafa kwa  mustakabli  wa kisiasa, kijamii na kiuchumi ambaye ameshajitolea kuwatumikia wananchi wenzake.

Alisema Dk. Mwinyi ni kiongozi aliyekuwa na maarifa ya kutosha ,aliyepevuka kifikra , kiakili na kisiasa huku akiizijua vyema  medani za utawala  chini ya uiongozi bora na mzalendo aliyejitolea  kutetea umoja na  utaifa.

Aidha alisema aghalab akiwa jukwanai  huzungumzia sera ,akitaka  misingi  ya nchi ,tunu na maadili ya Taifa yalindwe huku akiahidi utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi mwaka 2020/2025.

“Anaeleza kwa ufasaha tofauti  na wagombea wengine .Yeye hujenga nguvu ya hoja  na kutaja malengo ya kimaendeleo .Anagahamu mafanikio yaliofikiwa ,changamoto zilizopo na jinsi atakavyozitatua. Hapendi  urasimu,uvivu na uzembe  “Alisema