NA HUSNA SHEHA

MAHAKAMA ya Wilaya Mfenesini imempeleka Chuo cha Mafunzo, Amos Tomas Mapindu (30) mkaazi wa Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja, kwa muda wa miezi minane kwa kosa la wizi wa mazao.

Hakimu  Nyange Ali Makame, alitoa adhabu hiyo kwa mshitakiwa huyo, baada ya kulikubali kosa lake, mara  baada ya kusomewa na Mwendesha Mashitaka wa Serikalia kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka  Zanzibar, DPP  Ali Juma ndipo mahakama ilimtia  hatiani.

 Hakimu Nyange, alitoa adhabu hiyo  ili iwe funzo kwake na  wengine wenye taabia kama hiyo, ambapo kijana huyo alidaiwa kuiba Nazi tisa zenye thamani ya shilingi 4500 kwa makisio ,mali ya Faki Mussa, jambo ambalo ni kosa kisheria.

Alidaiwa kufanya wizi huo Septemba 25, mwaka huu majira ya saa 2:30 asubuhi huko Bumbwisudi kwa goa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani hapo ilidaiwa kuwa kitendo cha wizi wa mazao ni kosa kinyume na kifungu cha 251 (1) na 268 (1) (2) (3) vya sheria namba 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.

Baada ya kusomewa shitaka mshitakiwa alikubali kosa lake,ndipo mahakama ikamtia hatiani, huku upande wa mashitaka kudai kwamba hakuna kumbu kumbu ya makosa ya nyuma kwa mshitakiwa huyo, nakuiomba mahakama itowe adhabu kwa mujibu wa kosa lake.

Kabla ya mahakama kutoa adhabu mshitakiwa aliimbia mahakama impunguzie adhabu kwa vile ni mgeni wa mahakama.

Amos Tomas Mapindu, ameeanza kutimikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi minane kwa kosa la wizi wa Nazi.