NA ANTHONY ISHENGOMA, SHINYANGA

TUME YA Taifa ya Uchaguzi NEC imewatoa hofu wapiga kura wote wenye mahitaji maalumu kwa kutoa maelekezo kwa watendaji wa uchaguzi kutoa kipaumbele kwa watakaojitokeza kupiga kura wakati wa siku ya uchaguzi.

Makundi hayo ni watu wenye ulemavu, wajawazito , akina mama wanaonyonyesha ikiwemo wazee na wagonjwa,   ulemavu wa macho ambao watawekewa kifaa cha maandishi ya nukta nundu kwa kila kituo kwa wenye uwezo wa kutumia kifaa hicho, lakini pia wale wasioweza kuambatana na mtu wanayemwamini ili kuwasaidia kupiga kura. 

Akiongea wakati wa Kikao cha Wadau wa Uchaguzi wa Mkoa wa Shinyanga  Mkoani Shinyanga Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria NEC, Leonard Baraka, ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema Tume imetoa ruhusa kwa wasiojua kusoma na kuandika waruhusiwe kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura.

Aidha Baraka ameongeza kuwa Tume inasisitiza umuhimu  wa vyama vya  siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeini zao ikiwemo kuepuka lugha za kashfa na maneno ya uchochezi yanayotishia usalama na amani ya Nchi.

Wakati huohuo Afisa kutoka Tume ya Uchaguzi,  Nuru Riwa Kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia liongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Nchini amesema kuwa Walemavu waliojiandikisha kupiga kura ni ni takribani 13 elfu.

Aidha Kiongozi huyo wa Tume ya Uchaguzi amewataka wagombea na vyama vyao kuepuka kufanya kampeini ambazo zina viashiria vya ubaguzi katika misingi ya jinsi, ulemavu, ukabila, udini,maumbile au rangi.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Walemavu Mkoa wa Shinyanga Mzee Richard Mpongo ameomba Tume ya Uchaguzi kuwata wagombea kuweka wakalimani kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kusikia, ili nao waweze kujua wagombea wao wanaongea nini wakati wa kunadi sera zao.