WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema anajisikia kuwa na katika hali nzuri kiafya na hatumii tena dawa yoyote baada kuambukizwa na kuugua corona zaidi ya wiki moja.

Katika mahojiano yake kwa njia ya simu na kituo cha televisheni Fox, Trump, alisema, “nimevishinda virusi hivi vibaya vya China, ni kama nina kinga ya mwili kwa muda mrefu, muda mfupi, labda maisha yangu yote.”

Katika mahojiano hayo, mwanahabari hakumuuliza iwapo vipimo alivyfanyiwa vimeonesha kuwa hana tena virusi hivyo, ambavyo vimesh poteza msiha ya wamarekani zaidi ya 200,000 na kuambukiza zaidi ya millioni saba nchini Marekani.

Lakini muda mfupi baada ya kumaliza mahojiano na televisheni hiyo, Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, kwamba madaktari wake wamethibitisha kuwa amepona kabisa corona, hivyo hivi sasa hawezi kuambukizwa, wala kuwaambukiza watu wengine.

Baadae kampuni ya Twitter ilisema “ujumbe wa Trump unakiuka maadili ya mtandao wa Twitter kuhusu kusambaza habari za uongo, na kupotosha za janga la covid-19.