NA ABDI SULEIMAN

BENKI ya NMB tawi la Pemba imewaomba  wadau wake kuendelea kufurahia huduma zinazotolewa na banki hiyo.Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa benki hiyo Pemba, Hamad Msafiri, wakati wa halfa fupi ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, iliyofanyika Chake Chake.

Alisema benki hiyo imesaidia jamii kwa kutoa vitu mbali mbali, ikiwemo bati, nondo, saruji na madawati pale jamii inapopeleka maombi yao.

Aidha aliwashukuru wateje wao na Watanzania wote kwa kuendelea kuwaamini.Pia aliweza kuzindua huduma tatu za kidigitali zenye lengo la kurahisisha mawasiliano kati ya benki na wateja, ili kutoa huduma bora kwa wakati.

Alizitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na namba maalumu ya Whatsapp +255 747 333 444 kwa jili ya mteja anaetaka ufafanuzi wa hudma zao, QR Code ambayo inatoa nafasi kwa wateja wao kutoa maoni na mapendekezo ya uboreshaji wa huduma na  kurudisha tokeni ya LUKU kwa wateja wanaonunua umeme kupitia NMB mkononi.

Msaidizi Meneja wa benki hiyo, Omar Said, aliwaomba wananchi kuwa na utaratibu wa kukata bima kwani benki hiyo tayari imeanza kutoa huduma za bima.

Mmoja ya wadau wa benki hiyo, Massoud Ali Mohamed, aliitaka NMB kufika vijijini kutoa elimu ya ukataji bima pamoja na huduma mbali mbali wanazozitoa.

Alisema benki ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi, ili kusaidia jamii pamoja na kuwataka kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.