NA MWAJUMA JUMA

NUSU fainali ya michuano ya wazi ya mpira wa Kikapu inaanza kesho katika uwanja wa Mao Zedong mjini hapa.

Nusu fainali hiyo inatarajiwa kuchezwa saa 10:00 za jioni kwa mchezo ambao utawakutanisha kati ya JKU na Nyuki.

Mbali na timu hizo pia timu za Polisi na Stone Towne nazo zimeingia hatua hiyo na zitarajiwa kushuka dimbani kesho saa 10 za jioni.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha mchezo huo Zanzibar Rashid Hamza alisema michuano hiyo inaendeea vyema mpaka hatua hiyo ambayo imefikia.

Alisema  katika michuano hiyo changamoto kubwa ni kukosekana kwa wafadhili na nyengine zilizobakia ni za kawaida.

“Tunashukuru mpaka sasa tumeenda vizuri na changamoto kubwa ambayo ipo ni hiyo ya kukosekana kwa wafadhili”, alisema.

Hata hivyo alisema kwa upande wa wanawake wamebakia na mchezo mmoja ambao utawakutanisha JKU na KVZ .

Alisema mchezo huo ni wa kutafuta bingwa ambapo yoyote yule atakaeshinda atakuwa bingwa wa michuano hiyo ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuhamasisha amani kuelekea uchaguzi mkuu 2020.