NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya  Nyuki wanaume na JKU wanawake zimetwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Kamishna Cup, iliyomalizika juzi visiwani Zanzibar.

Timu hizo ambazo zilishiriki ligi hiyo kila mmoja ilishuka katika uwanja wa Mao Zedong kwa nyakati tofauti, ambapo Nyuki waliibuka kidedea hicho kwa kuifunga Polisi pointi 64-58.

Kwa upande wa JKU ambao fainali yao ilichezwa awali uwanjani hapo walifanikiwa kutwaa nafasi hiyo kwa kuwafunga wapinzani wao wa jadi timu ya KVZ .

Mchezo wa fainali uliowakutanisha Polisi na Nyuki ulioonesha ushindani mkali uliowafanya wengi wa mashabiki waliokuwepo wakifuatilia kuvutiwa nao.

Katika mchezo huo mgeni rasmi alikuwa Kanali Salum Lugoba ambae alimwakilisha Bregedi kamanda Bregedia ya Nyuki 101 KV.

Mashindano hayo ambayo yalikuwa yakishirikisha timu za wanawake na wanaume mabingwa wote walipatiwa zawadi ya vikombe.

Aidha kulitangazwa zawadi ya wachezaji bora kutoka kila upande ambapo kwa upande wa wanaume ni Nassor Haji Golo wa Nyuki na kwa wanawake ni Dawa Abdalla  wa JKU ambao walipewa zawadi ya cheti pamoja na kikombe kidogo.