NA ASIA MWALIM

JAMII imeshauriwa kujitokeza kuomba nafasi za kulea watoto wenye mahitaji maalumu ikwemo waliotelekezwa na familia zao ili kuboresha maisha ya watoto hao.

Ushauri huo umetolewa na Ofisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja, Fatma Othman Makenzi, alipokua akitoa mafunzo ya walezi kwa wananchi wa shehia ya Fuoni uwandani wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja.

Alisema kumekua na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao hukosa malezi bora ya baba na mama, hivyo kuwanyima haki zao za msingi na kuwanyima kutimiza ndoto zao za maisha.

“Kuna watoto hawajui wazazi wao wamekuwa kwenye nyumba za Serekali wanalelewa huko baada yaw a samariaya wema kuwaokota” alisema.

Aidha alisema endapo watoto watapatiwa mahitahi ya msingi, itasaidia kutatua changamoto zao ikiwemo kupatiwa elimu bora kwa wakati wake.

Alifahamisha kuwa kufanya hivyo kutaweza kuwajenga watoto kisaikolojia, kiakili na hata kujiona wana nafasi katika jamiii kama watoto wengine kutokana kuwaweka katika mazingira mazuri.

Nae Mratibu wa Wanawake na Watoto shehia ya Fuoni uwandani Husna John Pantaleo, alisema wametoa elimu ya mafunzo ya walezi wa walezi ndani ya shehia hiyo, ili kuwataka wenye uwezo waweze kujitokeza kulewa watoto.

Aidha mratibu huyo alisema lengo la kufanya mafunzo hayo ni kusaidia makundi ya watoto waliokumbwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kudhalilishwa, kutupwa, na kutelekezwa na familia zao ili kupatiwa huduma za msingi ikiwemo afya.

Alifahamisha kuwa malezi hayo yatachukua muda mrefu au mfupi, hii ni kutokana na aina ya tatizo lililompata mtoto husika lita gharimu muda gani.

Kwa upande wa wananchi waliopewa mafunzo hayo waliupongeza mradi huo ambao utaweza kuwapa watoto furaha ya kujihisi wapo katika mazingira salama.

Alieleza kuwa watoto wanapata fursa ya kubadilishana mawazo hujisikia faraja juu ya jitihada wanazozifanya kwenye masomo yao pale wanapokutana na watoto wengine wanaoishi katika mazingira tofauti.