KWA miaka na dahari, vitabu vitakatifu vinavyoelezwa kuwa vimetoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuja kuwaongoa waja wake, vimekataza kabisa mahusiano ya jinsia moja.

Katika kukazia suala hilo, baadhi ya nchi hapa ulimwenguni zimekuwa na sheria kali katika kuzuia mapenzi ya jinsia moja, hata hivyo nchi hizo wakati mwengine zinajukuma kwneye wakati mgumu kutoka kwa mataifa yenye kukubalina na mahusiano ya kijinsia.

Moja ya dhehebu la kidini hapa duniani ambalo linaonekana limekuwa gumu kukubaliana na mahusiano ama ndoa za jinsia moja ni kanisa katoliki, ambapo makao makuu yake yapo mji wa Vatican uliopo katika jiji la Rome nchini Italia.

Hata hivyo hivi karibuni na katika hali ya kushangaza sanam kiongozi wa kanisa hilo papa Francis, ameonekana kama vile yupo tayari kanisa lake likubaliane na kuunga mkono suala la mahusiano ya jinsia moja.

Kwa mjibu wa matamshi ya kiongozi huyo yaliyonukuliwa kutoka kwa video mpya ambayo imetolewa hivi karibuni, amesema kwamba watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja wanastahili kulindwa na sheria za mahusiano.

Taarifa ya papa ambayo imeandikwa na kuchapishwa na vyombo kadhaa vya habari vya kimataifa, ilieleza kwamba anafikiria wapenzi wa jinsia wanastahili kuruhusiwa kuoana.

Wachambuzi wanasema kauli yake hiyo imeashiria wazi msimamo wake kuhusu uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsia moja, katika makala yaliyoelekezwa na Evgeny Afineevsky.

“Watu wanaoshirika mapenzi ya jinsi moja wana haki ya kuwa na familia,”alisema katika filamu, ambayo ilioneshwa kwa mara ya kwanza Oktoba 21 mwaka huu.

“Ni watoto wa Mungu nawana haki ya kuwa na familia, hakuna mtu anayestahili kutengwa ama kufanywa ajihisi mnyonge kwa kuamua kuwa katika uhusiano wa aina hiyo. “Tunachopaswa kuunda ni sheria ya umoja wa kiraia ili kuwalinda kisheria”, alisema.

Aliongeza kwamba aliunga mkono wazo hilo, akiashiria nyakati alipokuwa askofu mkuu wa jiji la Buenos Aires huko Srgentina, akisema japo alipinga ndoa ya wapenzi wa jinsia moja katika sheria, aliunga mkono ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja.

Filamu ya Francesco, inayoangazi maisha na kazi ya papa Francis, ilioneshwa kama sehemu ya tamasha la filamu la Roma.

Japo kauli ya Papa kuhusu ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja iliangaziwa, filamu hiyo pia inamuonyesha akiwahimiza wanaume wawili mashoga kuhudhuria kanisani na watoto wao watatu.

Muandishi wa biografia ya papa Francis, Austen Ivereigh, alisema kwamba hakushangazwa na kauli ya hivi karibuni ya kiongozi huyo juu ya kuunga mkoni mahusiano ya jinsia moja.

“Huo ulikuwa msimamo wake alipokuwa askofu mkuu wa Buenos Aires,” alisema Ivereigh. “Siku zote alikuwa akipinga ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, lakini aliamini kanisa linapaswa kutetea sheria ya kuwalinda wapenzi wa jinsia.”

Chini ya mafundisho ya sasa ya katoliki, uhusiano wa wapenzi wajinsia moja unachukuliwa kama tabia potofu na isiyokubalika.

Mwaka 2003, shirika la mafundisho la Vatican, usharika wa mafundisho ya imani, lilisema kwamba heshima kwa watu wa jinsia moja haiwezi kwa njia yoyote kuidhinisha ya uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja au kutambuliwa kisheria kwa vyama vya wapenzi wa njinsia moja.

Tamko la Papa la hivi karibuni ni msururu wa maoni ambayo ametoa kuhusu haki za wapenzi wa jinsia moja, akiangazia msaada wanaostahili kupewa, lakini hajaidhinsha moja kwa moja mahusiano ya kimapenzi ya aina hiyo.

Mwaka 2013, katika kitabu cha Heaven and Earth, Papa alisema kuwa kusawazisha kisheria mahusiano ya jinsia moja na ndoa za jinsia moja itakuwa “upungufu wa kianthropolojia”.

Pia alisema ikiwa wanandoa wa jinsia moja wataruhusiwa kuasili, “watoto huenda wakaathitika … kwami kila mtu anahitaji kuwa na baba wa kiume na mama wa kike ambao wanaweza kuwasaidia utambulisho wao”.

Mwaka huo huo, alisisitiza msimamo wa kanisa kwamba vitendo vya ushoga ni dhambi, lakini akasema mwelekeo wa ushoga sio.

“Ikiwa mtu anashiriki mapenzi ya jinsia moja na anamtafuta Mungu kwa nia njema, mimi ni nani nimhukumu?,”aliuliza.

Mwaka 2014 iliripotiwa kuwa Papa Francis aliashiria kuunga mkono ndoa ya wapenzi wa wa jinsia moja katika mahojiano, lakini ofisi yake ya mawasiliano ilikanusha taarifa hizo.

Na mwaka 2018, Papa Francis alisema “ana hofu” kuhusu mapenzi ya jinsia moja miongoni mwa makasisi akiongeza kwamba ni “jambo zito”.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa msimamo huo wa papa wa kuunga mkono mahusiano ya jinsia moja umekosolewa vikali na makasisi wahafidhina wa kanisa hilo.

Mmoja wa viongozi wa katoliki waliomjia juu papa ni askofu Thomas Tobin wa Providence, makao makuu ya jimbo la Rhode Island la Marekani ambaye alisema tarifa ya papa inapingana wazi wazi na mafundisho na msimamo wa muda mrefu wa kanisa katoliki.

Askofu Tobin alisisitiza kuwa, kamwe kanisa hilo halitaruhusu au kubariki uozo wa namna hiyo wa kijamii.

Mapema mwaka huu, kiongozi wa zamani wa kanisa katoliki duniani Benedict XVI alimtaka papa Francis kusitisha mpango wa kanisa katoliki wa kuruhusu wachungaji wenye wake kuwa makasisi na maaskofu wa kanisa hilo.

Mpango ambao papa Francis anauunga mkono kutokana na kile kinachosemekana kuwa ni kupungua idadi ya viongozi wa kidini katika baadhi ya maeneo ya dunia kwa sababu ya kubanwa na sheria ya kutoruhusiwa kuoa