NA ABDI SULEIMAN

BENKI ya Watu wa Zanzibar (PBZ) tawi la Wete, imeadhimisha siku ya wateja kwa kujumuika na wateja wao na kuwashukuru kwa kuendelea kuwa na imani na benki hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kaimu Meneja wa tawi hilo, Ahmed Abubakar Mohamed, aliwashukuru wateja kwa kuendelea kuwa na imani na benki hiyo na kuahidi kuwahudumia kwa hali na mali.

Alisema benki hiyo inatoa huduma mbali mbali kwa jamii, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na zenye uhakika.

Aliwaomba wananchi wa wilaya ya Wete na Micheweni, kuendelea kuitumia benki hiyo kwa kuweka fedha zao.

Khamis Ali miongoni mwa wateja wa benki hiyo, aliushukuru uongozi wa PBZ Wete kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.