NA TATU MAKAME

 SALUMALI Jafar (38) mkaazi wa Nungwi amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na pikipiki kijijini hapo Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mkoa wa Kaskazini Unguja, tukio ambalo limetokea Oktoba 8, mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Haji Abdalla Haji, alithibitisha tukio hilo wakati alikizungumza na Zanzibar Leo, ambapo alisema marehemu kabla ya kifo chake alikuwa akitembea kwa miguu akitokea upande wa Kendwa kuelekea Nungwi, ndipo ilipotokea Honda aina ya pikipiki yenye namba za usajili Z. 895 KJ aina ya WATCO yenye rangi nyekundu kumgonga mwenda kwa miguu.

Alisema Honda hiyo, ilikuwa ikindeshwa na Mohamed  Makame Muhamed, (18) mkaazi wa Nungwi akiwa amewapakia  Abubakari  Abdala Abdalla  (15) na  na Issa  Haji Kombo wote wakaazi wa Nungwi ambao  ni wanafunzi wa darasa la  kumi wa skuli ya Nungwi  walikuwa wakitokea Kendwa Kuelekea kijiji hicho na ndipo alipomgonga mwenda kwa miguu na kumsababishia kifo.

Hata hivyo, Kamanda huyo, alisema mtuhumiwa atafikishwa kwenye vyombo vya sheria taratibu zitakapokamilika na sasa yupo chini ya ulinzi.