LONDOND, England
KIUNGO wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba, anataka kujiunga na Barcelona kwa uhamisho huru dirisha lilajo la majira ya joto.

Lakini, kwa kuzingatia hali ya sasa ya uchumi na kupunguza kwa mapato ambayo Barcelona imepata kutokana na janga la ‘corona’, sekretarieti ya kiufundi ya miamba hiyo inafahamu kuwa watapata mapungufu mengi ya kiuchumi wakati wa kumsaini, kama ilivyotokea katika usajili uliofungwa mnamo Oktoba 5.

Kwa sababu hiyo, wanatarajia kuwapata wachezaji kwenye soko linalowakabili wakati wa mwisho wa mkataba na inaonekana kuwa muhimu zaidi kuliko hapo awali.

Kuna nyota wawili mashuhuri ambao wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu wa sasa na bado hawajasainia klabu zao akiwemo pia David Alaba.

Beki huyo wa Bayern amekuwa kwenye ajenda ya Barca mara kadhaa na kwa sasa anapendelea kutofanya upya mkataba na Wajerumani endapo chaguo la kusaini Barca au Madrid litaonekana.
Pogba, kwa upande wake, pia anatajwa na Wakatalunya katika siku zijazo. Sergio Aguero, Di Maria, Oriol Romeu na Juan Bernat nao wanamaliza mikataba yao.(Goal).