KAMPALA,UGANDA

POLISI  nchini Uganda wataajiri maofisa maalumu wa Polisi 50,000 (SPCs) kwa Uchaguzi Mkuu wa 2021.

SPC 5,000 zaidi watajiunga na jeshi la polisi la kawaida.hatua ambayo  itachukua nguvu ya polisi ya sasa, ambayo iko karibu 44,000, kwa wafanyakazi wapatao 100,000.

Fred Enanga, msemaji wa polisi,alisema Askari hao watasaidia Jeshi kwa kuzingatia sheria, na watavunjwa baada ya uchaguzi.

“Tuna mipango ya kuajiri askari polisi maalumu wa uchaguzi kwa polisi madhubuti wa kipindi cha uchaguzi na kipindi cha baada ya uchaguzi,” Enanga alisema.

“Watafanya kazi kwa kipindi cha uchaguzi tu na watalipwa posho ya Sh375,200 kwa kila mtu,” akaongeza.

Enaga alisema kikosi hicho, ambacho kitaajiriwa kutoka kote nchini, kitatumwa mwezi mmoja kabla ya uchaguzi hadi kipindi kitakapomalizika na watasajiliwa kutoka mikoa tofauti kufanya kazi katika Wilaya zao.

Enanga alisema Polisi hawatowapeleka katika skuli ya mafunzo kama Kabalye.Sharti ikiwa ni kwamba lazima uwe raia wa Uganda, uwe na kitambulisho cha kitaifa, usiwe na rikodi ya jinai, uwe na umri kati ya miaka 18 hadi 40 na rikodi ya kuthibitishwa ya kujitolea na polisi.

Alisema pia polisi waliwaamuru makamanda wa polisi wa tarafa  wilaya, makamanda wa polisi wa mkoa na maofisa uhusiano kuwasiliana na viongozi wa wilaya kuhamasisha na kuwatambua wagombea wanaofaa wa kuajiriwa.

Tume ya Uchaguzi inatarajia kuwa wilaya zitakua hadi 141 ifikapo 2021, kutoka 121 mnamo 2016, wakati manispaa yataongezeka kutoka 39 hadi 80, kaunti ndogo kutoka 1,398 hadi 2,000 na parokia kutoka 7,431 hadi 9,500.

Vijiji pia vitaongezeka kutoka 57,842 hadi 65,200 na vituo vya kupigia kura vinatarajiwa kuongezeka hadi 35,000 kutoka 28,010 kufikia 2016.

Mamlaka ya polisi inasema wanahitaji nguvu kazi ya kutoa usalama katika maeneo yote na kuhakikisha utulivu.