KAMPALA, UGANDA

KATIKA hali isiyo ya kawaida, mwanasiasa kijana nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, amesema nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya uteuzi wa kugombea urais nchini zimepotea ofisini kwake.

Bobi Wine mbaye ni mwanamuziki maarufu nchini humo, alisema nyaraka hizo zinazohiajika kama miongoni mwa masharti ya kuwania urais zimepotea mara baada ya ofisi yake kuvamiwa na vikosi vya usalama.

Moja ya masharti la Tume ya Uchaguzi nchini Uganda ni kwa mgombea kuwasilisha kuwasilisha sahihi za wafuasi 100 waliojisajiliwa kama kupiga kura kutoka katika alau theluthi mbili ya wilaya za Uganda.

Mwanasiasa huyo machachari anayeutikisa utawala wa Museveni alisema kuwa timu yake tayari ilikwisha kusanya sahihi milioni sita tayari kuziwasilisha tume ya uchaguzi, lakini zimepotea.

“Serikali ya Museveni inajaribu kunizuwia kuteuliwa kama mgombea wa urais, kuanzia kuhoji nyaraka zangu, kuhoji umri wangu na sasa wanafanya kila juhudi kukwamisha uteuzi wangu na ninaamini kuwa ndio maana walichukua saini”, alisema Bobi Wine.

Kiongozi huyo ambaye amethibitisha kuwa atagombea kwenye uchaguzi utakaofanyika mwakani, alisema tukio hilo halitamkatisha tamaa ambapo amekwisha ripoti katika matawi yetukuhakikisha wanaanza kukusanya saini haraka uwezekanavyo.

Bobi Wine ambaye ni mbunge alizungumza na vyombo vya habari baada ya kufanikiwa kuvitoroka vikisi vya usalama wakati vilipovamia ofisi yake hapo juzi.

Aidha alisema kiasi cha shilingi milioni 23 zimeibiwa pesa ambazo zilichangiwa na wananchi wa Uganda kwa ajili kuwaidia wagombea wa ubunge.

Msemaji wa tume ya uchaguzi nchini Uganda, alisema hawezi kuzungumzia juu ya madai ya Bobi Wine ya kutoweka kwa nyaraka, lakini akasema muda wa mwisho unaweza uongezwa kwa mgombea.