NA MWANAJUMA MMANGA
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mjini Unguja, Awadh Juma Haji, amewataka wenye boda boda na vyombo vya moto kuacha tabia ya kubandika stika za namba za gari za viongozi pamoja na kufunika bendera katika vyombo vyao.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na jumuiya ya boda boda huko Maisara mjini Unguja, ambapo alisema kufanya hivyo kunapelekea kufanya vitendo vya uhalifu na hata kupelekea uvunjifu wa amani.
Alisema iwapo mtu atabainika amefanya hivyo hatua kali itachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa na hadi sasa kuna magari matano tu ndio yaliyopewa ruhusa ya kubandika stika hizo kwa mujibu wa sheria.
Hivyo amewataka wenye boda boda kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua wahalifu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika hivi karibuni na kutokubali kushawishiwa na kurubuniwa na viongozi wa vyama vya siasa wasiopenda maendeleo ya nchi.
Pia aliwasisitiza wakati wanapokwenda katika kampeni kuepuka kufanya mihemko wakati wakiwa na vyombo vya moto na fujo, ili ambayo inachangia uvunjifu amani.
Akizungumzia suala la usalama barabani, alisema umekuwa na ajali nyingi zinatokea hasa vyombo vya maringi mawili huwa ambazo zinatokea na kusababishwa na kutotii sheria na uzembe wa madereva kwa wanaoendesha.
“Tumekuwa na vijana wengi wanapoteza maisha ambao ni waendeesha vyombo vya maringi mawili lakini pia ambao ni watumiaji wa vyombo hivyo na wengine wanatumia barabara.