Joto la uchaguzi nchini Tanzania linazidi kupanda ambapo taifa hilo la Afrika Mashariki linafanya uchaguzi wake wa tano tangu kuasisiwa kwa demokrasia ya vyama vingi zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Watanzania wapatao Milioni 29.75 leo October 28, 2020 wameanza kupiga kura kuchagua Rais, Wabunge, Wawakilishi, na Madiwani watakaoongoza kwa miaka mitano ijayo.

Wapiga kura wana hadi mwendo wa saa kumi jioni kupiga kura,Matokeo yanatarajiwa kutangazwa ndani ya juma moja .