LUANDA, ANGOLA

RAIS wa Angola Joao Lourenco alisema ataffufua upya uchumi wa nchi hiyo na kupambana na umaskini.

Hatua hiyo ni moja sera zake za utawala mpya baada ya nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kudorora kwa uchumi wake kwa miongo kadhaa.

Katika hotuba yake, rais huyo alisema kuwa uchaguzi wa ndani utafanyika kwa mara ya kwanza nchini humo na kuthibitisha kujitolea kwake kwa utekelezaji wao.

Lourenco pia aliangazia vita dhidi ya ufisadi na kuahidi kuendelea kutilia maanani sana ujumuishaji wa demokrasia na utawala wa sheria.

Alisisitiza kwamba serikali ya Angola itaendelea kulipa kipaumbele suala la ugonjwa wa COVID-19, hata hivyo, itazingatia sana hali ya uchumi sambamba na ongezeko la uzalishaji wa ndani.

Kulingana na rais, serikali ilitumia zaidi ya milioni 300 kwa uagizaji wa chakula ikilinganishwa na mwaka 2019, ikisisitiza kuwa nchi hiyo imepanga kuongeza uwezo wake wa uzalishaji wa unga wa ngano mara mbili, kutoka tani 600,000 hadi 1.2 milioni mnamo mwaka 2021.

Aidha alisema takriban ajira 19,000 zimeundwa katika miezi ya hivi karibuni na kampuni na vituo vya ajira.