MADRID, Hispania
REAL Madrid inaweza kuhamia kwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Haaland, ikiwa itashindwa kuinasa saini ya Kylian Mbappe kutoka PSG ambayo imekuwa ikiitamani tangu msimu uliopita.

Hata hivyo ilishindwa baada ya uchumi kuyumba kutokana na janga la corona. Madrid imekuwa ikihaha kujenga safu ya ushambuliaji ambayo imepwaya tangu kuondoka kwa Cristiano Ronaldo huku Karim Benzema umri wake ukionekana kupepea.
Haaland anaangaliwa kama mbadala wa Mbappe ambaye ndio chaguo la kwanza, lakini, kuna uwezekano PSG isiwe tayari kumuachia na ikiwa itamuuza, itakuwa kwa fedha ndefu.

Mkataba wa Haaland unatarajiwa kumalizika mwaka 2024 na bei yake huenda ikawa rahisi ukilinganisha na ile ya Mbappe ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2022.(AFP).