NA ZAINAB ATUPAE

OFISA wa habari wa timu ya soka ya Ruvu Shooting Masau Bwire amesema watarudi tena Zanzibar kwa ajili ya kuanzisha tawi la Ruvu Shooting na kupata wanachama wa timu hiyo waliopo Zanzibar.

Ruvu ilikuja Zanzibar kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Jang’ombe Boys na kuondoka na ushindi wa mabao 3-1.

Alisema kuna haja kubwa ya kurudi visiwani Zanzibar kuweka tawi maalumu litakalo tumiwa na wanachama wa timu hiyo.

 “Ruvu Shooting ni moja kati ya timu kubwa ambayo inatambulika, kuja Zanzibar kufungua tawi letu na sisi tukawa na wanachama wengi ambao tutashirikiana nao kwenye mambo mbali mbali,”alisema.

Alisema malengo yao ni kushiriki kombe la Mapinduzi,hivyo kupata watu ambao watatupa mashirikino wakati wa mashindano hayo.

 “Tumekua na kawaida ya kwenda mikoa tofauti tofauti kwa lengo la kuonana na mashabiki wetu na kuanzisha matawi kwa Tanzania Bara, na Zanzibar tutaka tufanye kama hivyo”alisema.