ZASPOTI
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limeithibitisha Rwanda kuwa mwenyeji wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 mwaka huu.
Nchi tisa zitashiriki katika mashindano hayo ya wiki mbili, yaliyopangwa kufanyika kuanzia Disemba 13-28.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kuanzia Novemba 22 hadi Disemba 6.
Mashindano yote mawili ya kikanda yatakuwa kama ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) katika umri huo.

Katika mkutano wa Cecafa wiki iliyopita, Oktoba 10 huko Arusha, Tanzania, ilikubaliwa kwamba ujumbe wote, wachezaji, makocha na wafanyakazi watafanyiwa uchunguzi wa ‘corona’ kabla ya mashindano kama hatua za usalama dhidi ya janga hilo.
Rwanda haijajitokeza kwenye fainali za AFCON U-20 au U-17 tangu kuandaa mashindano ya mwaka 2009 na 2011, mfululizo.

Wakati kikosi cha Amavubi chini ya umri wa miaka 20 kikiondolewa kutoka kwenye mashindano hatua ya makundi, vijana wa U-17 wa Amavubi walijikuta wakifikia fainali walipofuzu Kombe la Dunia la U-17 la Fifa la 2011, lililofanyika Mexico.
Kufikia sasa, Rwanda inabakia kuwa nchi pekee ya Cecafa kuwahi kushiriki katika Kombe la Dunia la Fifa.

Wakati huo huo, kulingana na taarifa, Rwanda haitashiriki michuano ya U-20 nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa), Regis Uwayezu, ameshindwa kueleza kwanini Rwanda itajiondoa kwenye mashindano hayo.

Mataifa yaliyothibitisha kushiriki michuano ya U-17 ni Burundi, Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Sudan, Eritrea, Djibouti, Ethiopia, Kenya na wenyeji Rwanda.
Kwa upande wa U-20 ni pamoja na Somalia, Burundi, Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Sudan, Eritrea, Djibouti, Ethiopia, Kenya na wenyeji Tanzania.(New Times).