KIGALI,RWANDA

MAMLAKA za mitaa, wakaazi na shirika la mwavuli wa vyama vya manusura wa mauaji ya kimbari, kwa pamoja wanafukua kaburi la umati linalosadikiwa kuwa na mabaki ya wahasiriwa wapatao 5,000 wa mauaji ya kimbari ya Rwanda katika Wilaya ya Gatsibo, mashariki mwa Rwanda.

Ofisa wa eneo hilo alisema uchimbaji wa kaburi la umati uliogunduliwa hivi karibuni katika tarafa ya Kiziguro kulingana na ushuhuda wa manusura wa mauaji ya kimbari ulianza Jumanne na inaweza kuchukua wiki tatu.

Meya wa Wilaya ya Gatsibo Richard Gasana aliiambia Xinhua katika mahojiano ya simu kwamba shimo hilo, ambalo liliripotiwa kuchimbwa miaka ya 1970 kwa ajili ya usambazaji maji, linakadiriwa kuwa na kina cha mita 30, alisema Gasana, na kuongeza kuwa ufukuzi huo umecheleweshwa kuandaa jamaa za wahanga.

Mamlaka  wamekuwa wakitoa rai kwa Wanyarwanda na habari ambayo inaweza kusaidia kutambua makaburi ya watu wasiojulikana ya wahanga wa mauaji ya kimbari kujitokeza.

Mabaki ya wahanga wa mauaji ya kimbari bado yanagunduliwa katika maeneo mengi ya Rwanda kwa zaidi ya miongo miwili baada ya mauaji ya kimbari yaliyoua zaidi ya watu milioni moja, haswa Watutsi.

Katika mwaka wa fedha wa 2018-2019, mabaki ya waathirika 118,049 yaligunduliwa katika wilaya 17 kote nchini Afrika ya kati, kulingana na Tume ya Kitaifa ya Kupambana na Mauaji ya Kimbari.