WAPENZI wasomaji wetu wa Zanzibar Leo ambapo leo nimewatayarishia SALADI YA QUINOA NA PARACHICHI.

Tutawafahamisha namna ya kutengeneza saladi ambayo ni muhimu sana kwa afya ya wanaadamu.Hivyo ni lazima kupata vipimo, namna ya kutayarisha nakadhalika.

Vipimo

Quinoa – vikombe 2

Parachichi  (Avocado) – 1

Pilipili boga jekundu – 1

Sosi ya saladi (salad dressing)

Mafuta ya zaytuni – ¼ kikombe

Chumvi kiasi

Ndimu – 1 kamua

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

Roweka kidogo quinoa kisha chemsha kidogo tu  kisha chuja maji na kamua.

Kisha weka katika bakuli.

Katakata parachichi, pilipili boga, weke uchanganye pamoja na quinoa ikiwa tayari kuchanganywa na dressing yake.

Sosi (Dressing ya saladi)

Changanya mafuta ya zaytuni, chumvi, ndimu ikiwa tayari kumiminwa na kuchanganwa na saladi