KIGALI,RWANDA

WIZARA ya elimu imeahidi kuongeza uwezo wa mwalimu Saccos kwa kuwakopesha walimu na kuboresha ustawi wao.

Hii ilitangazwa na Valentine Uwamariya, Waziri wa Elimu,wakati ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Walimu Duniani.

Kuboresha ustawi wa walimu kutasaidia sana katika kuinua ubora wa elimu inayotolewa nchini.

Walimu,haswa wa kibinafsi, ni wataalamu ambao waliathiriwa zaidi na janga la Covid-19 kufuatia kufungwa kwa skuli muda mrefu katika jaribio la kukabiliana na kuenea kwa virusi.

Kwa hivyo, kuongeza uwezo wa Saccos ya kukopesha pesa kwa wanachama wake itasaidia walimu wakati wa shida.

Ushirika wa akiba na mikopo ya mwalimu unaendelea kukabiliwa na shida za kifedha, ikidhoofisha uwezo wake wa kutekeleza jukumu lake.

Waziri alisema kuwa mwalimu Sacco inakabiliwa na ufinyu wa bajeti ya Rwf11 bilioni.

“Hapo awali,tulikuwa na mipango ya kuingiza Rwf30 bilioni lakini ni Rwf19 bilioni tu ndiyo ilitolewa ikiacha pengo la jumla ya Rwf11 bilioni” alisema waziri Uwamariya.

Alisema, hatua hiyo inatokana walimu kutoa malalamiko juu ya kutoweza kupata akiba na mikopo yao,wakiahidi kuingilia kati.

“Tunajua juu ya hili, na kwa kweli tunatafuta kuziba pengo hilo kwa sababu tunaelewa kuwa walimu wanakabiliwa na nyakati ngumu,”alisema Waziri.

Etienne Havugimana, mwalimu mkuu skuli ya Msingi ya Busuku ambayo iko Rutsiro, anasema kuwa malipo duni ndio sababu kuu kwa nini walimu wengi hawapati mikopo kutoka Saccos yao.

Havugimana alielezea kuwa ushirika hutoa mikopo kwa walimu kulingana na mshahara wao kwa riba ya chini ya asilimia 11 ikilinganishwa na mikopo kutoka kwa benki za biashara ambapo viwango vya riba vinazidi kati ya asilimia 14 na 20.

“Hii haitoshi kusaidia familia yake katika suala la malazi, usafiri kati ya mahitaji mengine ya kimsingi,”alisema.