NA FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi nchini limewaahakikishi watazamaji wa uchaguzi  wa nje ya nchi kuwa nchi ya Tanzania ni salama,hivyo watembee maeneo mbalimbali bila kuwa na wasiwasi wowote.

Hayo yalisemwa jana kwenye mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na watazamaji wa  uchaguzi kutoka ndani na nje ya nchi,  kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Akizungumza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)  Sirro, Alisema ukiwa mtazamaji haupo juu ya sheria ambapo unaweza kutoka nje, lakini usipofuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zilizopo nchini unaweza kujikiuta ukawa muhalifu ambapo sheri aitachukua mkondo wake.

“Pamoja ni wageni wamekuja kutazama uchaguzi wajitahidi sana wasivunje sheria bali wakivunja sheria ,sheria itachukua nafasi yake na wasilaumu”alisema

Alikumbusha watazamaji wa ndani wameshapewa nafasi na Serikali imeona unafaa kuwa mtazamaji hivyo wasivunje sheria na watende haki na kushauri jambo ambalo la haki na wasiingie kwenye ushabiki,kwani ukifanya hivyo utakuwa ni muhalifu.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo, alisema mkutano ni mzuri kwakuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekumbushwa kutimiza wajibu wao, na Jeshi wamekumbushwa wajibu wao pamoja na watazamaji wakumbushwa wajibu wao ambapo kila mdau akitimiza wajibu wake uchaguzi utakuwa wa amani.