BRUSSELS,UBELGIJI

KAMISHNA wa Masuala ya Kiuchumi wa Umoja wa Ulaya, Paolo Gentiloni amesema sheria za umoja huo ambazo zinaweka mipaka kwa serikali kukopa,zitaendelea hadi mwaka 2021 kutokana na kuporomoka kwa uchumi kulikosababishwa na janga la virusi vya corona.

Tangazo hilo limetolewa baada ya Gentiloni kukutana na mawaziri wa fedha wa nchi za ukanda unaotumia sarafu ya Euro mjini Brussels.

Sheria hizo ziliimarishwa kutokana na mzozo wa kifedha ulioikumba Ulaya mwaka 2009, kwa lengo la kuulinda uchumi wa umoja huo.

Gentiloni alisema uamuzi huo utaziwezesha serikali kuanzisha mipango mikubwa ya msaada kwa ajili ya uchumi, bila ya kuwa na hofu ya vikwazo kutoka Brussels.

Mapema mwaka huu,Halmashauri ya Ulaya inayosimamia utekelezaji wa sheria za fedha ilipunguza deni la umma kila mwaka, wakati ambapo uchumi wa Umoja wa Ulaya ukiingia kwenye rikodi ya kudorora.