RABAT, Morocco

BOUCHRA Hajij, raia wa Morocco amechaguliwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Wavu (Volleyball) la Afrika (CAVB).

Bouchra alipata kura 42 kumuondoa madarakani c aliyepata kura 12, katika uchaguzi uliofanyika jumapili kupitia mtandao. Elwani alishika wadhifa huo kuanzia mwaka 2001.

Wakati huohuo, Waithaka Kioni raia wa Kenya alitetea nafasi yake kwa kupata kura 38 na kumshinda mpinzani wake wa Kanda ya V Joseph Will wa Sudan Kusini aliyepata kura 10.