EDWARD Joseph Snowden, amezaliwa Juni 21 mwaka 1983 huko katika mji wa Elizabeth City, uliopo North Carolina nchini Marekani, akitokea katika familia iliyojengwa na mzee Lonnie Snowden na bibi Elizabeth Snowden.

Edward Snowden, tunayemzungumzia katika makala haya ni mtaalamu wa kompyuta na wakala wa zamani wa shirika la usalama wa taifa la nchini Marekani (NSA).

Baba yake ambaye ni mzee Lonnie Snowden hadi mwaka hadi 2009 alikuwa akilitumikia jeshi la Marekani akiwa katika kambi moja iliyopo Pennsylvania, wakati mama yake Elizabeth Snowden, wakili anayefanyakazi zake katika korti ya shirikisho huko mji wa Baltimore.

Hata hivyo, wazazi wa Edward Snowden waliachana, huku taarifa zikieleza kuwa Edward ana dada mkubwa, Jessica Snowden anayefanyakazi katika kituo cha mahakama cha shirikisho huko mjini Washington.

Alitumia utoto wake huko Elizabeth City, aliishi Maryland karibu na makao makuu ya shirika la ujasusi la taifa nchini Marekani (NSA) huko Fort Mead na mnamo mwaka 1999, yeye na familia yake walihamia rasmi Ellicott City, Maryland.

Snowden alisoma sayansi ya kompyuta katika chuo cha jamii cha Anne Arundel huko Maryland, lakini alishindwa kupata diploma kutokana na miezi kadhaa kushindwa kuhudhuria masomo kwa sababu za akiafya.

Baada ya kupona maradhi yaliyokuwa yakimsumbua alirejea chuoni kumaliza masomo yake ambapo alifanikiwa kufanya mitihani na kufauli vizuri sana.

Mei 7 hadi Septemba 28 mwaka 2004, Snowden ajiunga na jeshi la Marekani, na alizanza mafunzo ya awali ya kijeshi ili akifanikiwa kumaliza mafunzo hayo aweze kushiriki vita nchini Iraq.

Mwaka 2006, Snowden aliandika kwenye programu ya online inaohusisha wachakalikaji, Hackers na watengeneza hardware kwamba kupata kazi kwake si tatizo kwani yeye ni mchawi wa kompyuta.

Iliripotiwa na New York Times kwamba Snowden aliwahi kupata mafunzo ya Certified Ethical Hacker mwaka 2010 na kuelezea maisha yake kuwa ya kuridhika akiwa analipwa mshaharawa dola 200,000 kwa mwezi.

Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana alishindwa kumaliza mafunzo ya kijeshi   baada ya kuvunjika miguu yote wakati wa mazoezi ya mazoezi, bila kumaliza kozi ya jeshi.

Alifanya kazi katika shirika NSA, akianza kazi ya kulinda kituo cha siri katika Chuo Kikuu cha Maryland, Edward alikuwa na ufikiaji sio tu kwa siri ya juu, lakini pia kwa habari ya “ujasusi maalum” iliyo na maelezo ya kiufundi ya shughuli za ujasusi za Marekani na washirika wake.

Wakati alikuwa akifanya kazi kama msimamizi wa mfumo katika NSA huko Hawaii, Snowden aliwashawishi wenzake 20 hadi 25 wampe ‘logins’ na ‘password’ zao, akielezea kwamba alihitaji kufanya kazi.

Baada ya NSA, alifanya kazi katika idara ya usalama ya CIA, kutoka Machi 2007 hadi Februari 2009, alifanya kazi chini ya jalada la kidiplomasia la ujumbe wa kudumu wa Marekani kwa UN mjini Geneva. Kazi yake ilihusiana na usalama wa mitandao ya kompyuta.

Snowden anatizamwa kwa macho mawili kwanza anatizamwa kama shujaa, lakini mamlaka nchini Marekani zinamchukuliwa kama msaliti, hasa baada ya hatua yake ya kufichua nyaraka za siri kuhusu udukuzi wa kimataifa uliofanywa na shirika la ujasusi la NSA.

Snowden alivujisha siri kwa mara ya kwanza kwa mwanahabari Glenn Greenwald wa gazeti la The Guardian la London mwaka 2013 akiwa ameajiriwa kama mchambuzi wa njia za mawasiliano katika tawi la NSA.

Taarifa hizo zilichapishwa na habari za siri hizo Juni 2013 na kuweka wazi programu kama uingiliaji wa data za simu za Marekani na Uingereza ikiwa ni pamoja na programu kama The Prisma na Tempora ambayo inahusu mfumo wa ufuatiliaji wa taarifa kwa njia ya intaneti.

Ufichuzi huo uliofanywa na Snowden wa kutoa taarifa za kimawasiliano zilizokuwa zikichunguzwa na kuhifadhiwa na NSA, ulikuwa moja ya ufichuaji mkubwa zaidi katika historia ya Marekani.

Snowden alifichua taarifa kadhaa zinazohusu namna Marekani inavyochunguza taarifa zinazohusu mataifa kadhaa yakiwemo mataifa marafiki, kuchunguza taasisi, mashirika na watu mbalimbali mashuhuri.

Hatua hiyo ya kujiripua iliyochukuliwa na Snowden ilisababisha wanaharati duniani kote kughadhibika huku wakieleza kuwa kitendo hicho ni kinyume cha haki za binaadamu.

Snowden alinukuliwa akisema kwamba uvujishaji wa siri alioufanya ni juhudi za kuujulisha ulimwengu kuhusu mambo yanayofanyika dhidi ya wananchi. Uvujishaji wa siri wa Snowden unaelezewa kuwa moja ya matukio makubwa kabisa ya uvujishaji siri katika historia ya NSA.

Mpaka anaondoka Marekani mwezi Mei 2013, alikuwa akifanya kazi kwenye consulting firm inayojulikana kama Booz Allen Hamilton huko Hawaii kwa mshahara wa dola 122,000 kwa mwezi.

Wakati maofisa wa intelijensia wanadai Snowden alikuwa ‘system administrator’ yeye anadai alikuwa ni mchambuzi wa njia za mawasiliano (infrastructure analyst), ikimaanisha kazi yake ilikuwa ni kuingilia mifumo ya intaneti na simu ya dunia nzima.

Alisema kuwa alitafuta ajira NSA (National Security Agency), ili kuku sanya taarifa juu ya mifumo ya ufuatiliaji ya NSA dunia nzima ili avujishe taarifa hizo.

Snowden alisema kwamba katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2008, alikipigia kura chama kisichokuwa na nguvu ya ushindi na alikuwa akipanga kufichua siri kuhusu mifumo ya ufuatiliaji ya NSA wakati huo lakini aliamua kusubiri kwa kuamini katika ahadi za Obama.

Lakini baadae alisema alivunjika moyo moyo kuona kuwa Obama anaendeleza sera za aliyemtangulia George Bush.

Wakati anataka kuvujisha taarifa hizo nyeti, Snowden aliandika naelewa nitafanywa nijute na kuhangaika kwa matendo yangu na kurudisha taarifa kwa jamii kuna fanya mwisho wangu.

Snowden alielezea matendo yake kwa kusema “sitaki kuishi kwenye jamii ambayo inafanya matendo kama haya (serveline on its citizens), Sitaki kuishi kwenye dunia ambayo ambayo kila ninachofanya na ninachosema kina rekodiwa”, alisema.

“Sina nia ya kuficha, mimi nina sababu najua hakuna baya nililofanya”, na kuongeza kuwa anatumai kujitambulisha kwake amewalinda wenzake kuwindwa ili kujua nani ana husika na uvuzishaji huo.

Kitendo cha uvuzishaji wa siri kilicho fanywa na Snowden kilipokewa kwa hisia hasi na wabunge wa congress wakimuita Snowden msaliti na akamatwe na kushitakiwa.

Lakini mwakilishi Thomas Massie yeye alikuwa kati ya wachache walio hoji uhalali wa katiba kuhusu program ya uingiliaji wa mawasiliano na kupendekeza Snowden aonewe huruma.

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter alisema alichofanya Snowden ni uvunjaji wa sheria za Marekani, lakini tabia ya Marekani kuingilia mazungumzo na mifumo ya mawasiliano ya watu ni jambo ambalo limevuka mipaka.

Taasisi ya Gallup iliyofanya utafiti ilieleza kuwa asilimia 44 ya wamarekani waliona ilikuwa sawa kwa Snowden kushirikiana na vyombo vya habari kurusha taarifa wakati hizo, huku aidha asilimia 42 waliona alikosea kufanya hivyo.

Serikali za Ulaya zilikasirishwa na vitendo vilivyo fanywa na Marekani kuchunguza mawasiliano ya watu wake na kueleza kuwa ni mambo yasiyokubalika.

Baada ya kufanya tukio hilo akakimbilia nchini Urusi ambapo inaaminika hadi sasa anaishi huko, ili kukwepa mkono wa serikali ya Marekani akiwindwa kwa usaliti wake.

Mnamo Juni 14 mwaka 2013, waendesha mashitaka wa serikali ya Marekani walimtuhumu Snowden kwa wizi nyaraka za serikali na kuvunja sheria ya usalama wa taifa yam waka 1917.

Kwasasa Snowden ni mmoja ya watu wanaohitajika zaidi na Marekani, lakini ni ngumu kumdaka maana hata aliyekuwa mkurugenzi wa FBI James Comey aliwahi kusema, “Snowden akiwa CIA na NSA aliishi na magenius, lakini wote kwake walikuwa ni taka taka mbele ya Snowden”.

Alifanikiwa kukwepa mkono wa sheria wa serikali ya Marekani ambapo pamoja na paspoti yake kuharibiwa alipanda ndege na kutua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sheremetyevo uliopo Moscow nchini Urusi.

Kwa sasa jasusi huyo amepewa hifadhi na serikali ya Urusi akiwa anaishi nchini humo, huku Marekani ikihaha kumtafuta.