TOKYO,JAPAN

WAZIRI Mkuu wa Japani Suga Yoshihide ameahidi kufuatilia machaguo yote ili Japani ifikie kiwango cha sifuri cha utoaji gesi chafuzi kwa mazingira kufikia mwaka 2050.

Katika Baraza la Chini la Bunge, wabunge walimuuliza Suga juu ya hotuba yake ya sera aliyoitoa wiki hii.

Mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha Constitutional Democratic, Edano Yukio aliunga mkono mpango wa Suga wa kufikia jamii yenye kiwango sifuri cha kaboni kufikia mwaka 2050, lakini alimtaka kutoongeza utegemeaji wa nishati ya nyuklia ili kufikia lengo hilo.

Suga alisema serikali inalenga kuokoa nishati vilivyo na kuanzisha nishati mbadala kwa kiwango kikubwa ili kupunguza kiwango cha utegemeaji wa nishati ya nyuklia kadiri iwezekanavyo.

Suga aliongeza kwamba haitakuwa rahisi kufikia lengo hilo na kusisitiza  umuhimu wa jitihada zinazofanywa na sekta ya nishati inayowajibikia asilimia 80 ya gesi chafuzi.

Alisema serikali itafuatilia machaguo yote ikiwemo  nishati mbadala bali pia nishati ya nyuklia, na kuahidi mijadala mikali isiyokuwa na uamuzi uliofikiwa.