NA FATUMA KITIMA,DAR ES SALAAM

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mwanza imefanikiwa kuokoa gari moja aina ya Toyota Land cruzer lenye namba ya usajili T.824 BGY,pikipiki tatu aina ya ya DT 125 na fedha kiasi cha shilingi 55,561,800 katika kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu.

Akitoa taarifa hiyo jana Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Emmanuel Stenga, alisema kuwa Mali hizo zilizokolewa ilikuwa ni mali ya chama cha kutetea maslahi ya wakulima wa zao la pamba Tanzania (TACOGA).

Stenga alisema kuwa Desemba 23  mwak 2017, ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, katika mkutano wa wadau wa pamba uliofanyika mjini Shinyanga, ambapo alitangaza rasmi kuivunja Tanzania Cotton Growers Association (TAGOTA) kama  mwakilishi wa pamba.

Alisema Serikali inafufua ushirika kupitia vyama vya msingi na kupitia mifumo huo wakulima watapata mwakilishi katika masuala yote ikiwemo kuivunja TAGOTA Waziri Mkuu aliagiza mali zote zilizokuwa zinamilikiwa na chama hicho na zikabidhiwe na bodi ya pamba.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU Mkoa wa Mwanza umebaini kuwa agizo la Waziri mkuu kuivunja TACOGA lilitekelezwa na kwa sasa hakuna ofisi wala uongozi wa unaoishi .

Pia mali hazikukabidhiwa zote kwa bodi ya pamba kama ilivyoelekezwa na kwamba baadhi ya viongozi na watumishi waliendelea kushikilia na kutumia mali hizo ikiwemo gari  moja na pikipiki saba

“Kwasasa TAKUKURU mkoa wa Mwanza imefanikiwa kuokoa gari hiyo ambayo ilikuwa inatumiwa na aliyekuwa dereva wa TACOGA Emmanuel Zegezege pamoja  na pikipiki yenye namba T842  BHK iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa Katibu mkuu wa TACOGA George Mpanduji, pikipiki yenye namba MC 321 AGQ iliyokuwa inatumiwa na mjumbe wa kamati tendaji, Thereza Stephano, na pikipiki namba MC 343 AGQ iliyokuwa inatumiwa na mjumbe wa kamati tendaji Bakari Khamisi”alisema

Aidha wameujulisha umma kuwa operesheni hiyo bado inaendelea na kwa yeyote anayefahamu kuwa anamiliki mali za iliyokuwa TACOGA ajisalimishe mara moja katika ofisi ya TAKUKURU iliyo karibu nae na kufanya makabidhiano ya mali aliyonayo ,vinginevyo wahusika watakamatwa na sheria itachukua mkondo wake.

Pamoja na kuokoa mali hizo alifahamisha kwamba, TAKUKURU Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha Julai Septemba mwaka huu,ambapo imeokoa fedha kiasi cha shilingi 55,531,800  kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 2,451,00  zimewekwa kwenye akaunti maalum ya Serikali iliyopo benki kuu.

Alieleza kuwa kiasi cha shilingi 23,814,200 zimerejeshwa kwenye vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) na SACCOS Shilingi 17,968,600 zimereshwa kwa wananchi mbalimbali waliodhulumiwa kwenye mikopo ,jumla shilingi 10,071,000 zimerejeshwa .