KABUL, AFGHANISTAN

RAIS wa Marekani Donald Trump amepata uungwaji mkono usiokuwa wa kawaida katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa rais na Novemba 3, baada ya kuidhinishwa na kundi la wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid ameiambia televisheni ya Marekani ya CBS News katika mahojiano ya simu mwishoni mwa wiki kuwa wanatumai atashinda uchaguzi na kukamilisha mpango wa kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.

Lakini wanamgambo hao wa Taliban walielezea wasiwasi kuhusu Trump kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19, wakisema walikuwa na wasiwasi na afya yake.

Msemaji wa timu ya kampeni za Trump Tim Murtaugh alisema timu hiyo inakataa uungwaji mkono wa Taliban.

Aliambia CBS News kuwa Taliban wanapaswa kufahamu kuwa rais wakati wote analinda maslahi ya Wamarekani kwa njia yoyote ile.