NA MWANDISHI WETU

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania imekuwa mshindi wa Tatu kupata Tuzo za Taasisi zinazosimamia Biashara Duniani, 2020 (WTPO Awards 2020) katika kipengele cha matumizi bora ya ushirikiano (Best use of Patnership) katika huduma ya kliniki ya Biashara inayosimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Theresa Chilambo, alieleza kwamba,

Tuzo hizi zimetangazwa jijini Geneva nchini Uswidi ambapo Tanzania imewakilishwa  na Balozi Maimuna Kibenga Tarishi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa- Geneva. 

Tuzo hizo alisema zinazosimamiwa na kutolewa na Kituo cha Biashara cha Kimataifa Duniani (ITC), ili kutambua michango ya Taasisi zinazosimamia sekta ya biashara duniani (TPO) katika kusaidia Wafanyabiashara wadogo na kati (SMEs) kuimarisha uzalishaji bora wa bidhaa zao, kuwajengea uwezo wa kufanya biashara na kuweza kuuza bidhaa wanazozalisha nje ya nchi.

Alisema kwa mara ya kwanza Tanzania kupitia taasisi yake ya TanTrade imeweza kushiriki tuzo hizo katika kipengele cha matumizi bora ya ushirikiano kupitia huduma ya Kliniki ya Biashara.

Pia TanTrade alisema kwa ushirikiano wa Benki ya Biashara ya Tanzania (NBC) ambapo huduma hii inalenga kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara Wadogo, wa Kati na Wakubwa nchini.

Alisema  baada ya serikali kuwa na andiko la Blue Print, ili kujenga mazingira rafiki ya ufanyaji biashara na kuweza kufikia uchumi wa viwanda.