WASHINGTON,MAREKANI

RAIS wa Marekani Donald Trump na mshindani wake Joe Biden wamepambana katika mdahalo wa pili na wa mwisho kwenye mji wa Nashville katika jimbo la kusini la Tennessse.

Biden aliyekuwa makamu wa rais wa Marekani hapo awali,alisema Trump hafai tena kuwa rais wa nchi hiyo kutokana na vifo vya wamarekani zaidi ya laki mbili viliyvosabaishwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Alisema rais Trump hana mkakati wowote juu ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

Trump alijibu kwa kusema kwamba wamarekani wanapaswa kutoka nje na kufanya kazi.

Trump alisema lazima nchi iwe wazi,wakati zimebakia siku11 kabla ya uchaguzi, rais Trump anayewania muhula wa pili alijitetea juu ya madai ya kuwa na akiba ya benki nchini China.

Trump alisema akiba hiyo ya benki ni ya toka mwaka 2010 wakati alipokuwa mfanyabiashara.